Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa zilizoripotiwa na gazeti la Tanzania Daima la kila
siku kuhusu uwepo wa dawa zilizoisha muda wa matumizi kwenye duka la dawa la Core
Pharmacy jijini Dar es Salaam. Taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na mmiliki wa duka la
dawa la Shine Care Pharmacy kwenye gazeti hilo.
Baadhi ya dawa zilizotajwa ni Listerine
antiseptic mouthwash, Pimple Gel, Misoprostol tablets 200mcg, Rabeloc IV 20mg, Mefenamic
acidic tablets, Herpex – 800 DT, Inhaler 100 pg dose, Metformin Denk 850, Comprimes de
carvediola 12.5mg na Cloderm cream.
Aidha, taarifa zimedai pia kuwa TFDA pamoja na kufahamishwa suala hili haikuweza
kuchukua hatua zozote kwa mlalamikiwa.
TFDA inapenda kukanusha upotoshaji huo unaofanywa na chombo hicho cha habari
kutokana na ukweli uliopo. TFDA ilifuatilia suala hilo na kubaini uuzwaji wa dawa moja tu
ya Listerine antiseptic mouthwash (chupa 2) ambayo iliuzwa katika kipindi ambacho muda
wake wa matumizi ulikuwa umebaki mwezi mmoja. Taarifa zinazoendelea kutolewa na
gazeti la Tanzania Daima zinatokana na mgogoro uliopo baina ya makampuni mawili ya
kuuza dawa ya Core Pharmacy na Shine Care Pharmacy.
TFDA inauhakikishia umma kwamba iko makini na ina mifumo madhubuti ya kufuatilia
ubora, usalama na ufanisi wa dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba kwenye soko. TFDA
inaviasa vyombo vya habari pia kufanya uchunguzi wa kina na kufika ofisini kwake ili
kupata taarifa sahihi badala ya kutoa taarifa inazozipokea kutoka kwa wafanyabiashara.
Imetolewa na:-
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
EPI MABIBO EXTERNAL,
S.L.P 77150, DAR ES SALAAM
Simu: + 255 222 450512/450751/452108
Nukushi: + 255 222 450793
Barua pepe: info@tfda.or.tz
Tovuti: www.tfda.or.tz
No comments:
Post a Comment