HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 20, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI,WILAYANI NYASA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielekea eneo la jukwaa mara baada ya kuwasili katika eneo palipofanyika uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) wilaya ya Nyasa. Kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli
Rais Jakaya M. Kikwete akichukua mkasi kwa ajili ya kukata utepe tayari kuelekea katika eneo la uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, kulia kwake ni Waziri mwenye dhamana na nishati Prof. Sospeter Muhongo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa serikali wakiwepo Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli wakiwa wameshika utepe tayari kwa Rais kuukata na kuelekea kubonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi huo wa umeme.

Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe kwa ajili ya uzinduzi rasmi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad