Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Maryam Muhaji akizungumza jambo katika hafla ya kufuturisha wastaafu iliyofanyika katika hoteli ya Tanga Beach,Mkoa wa Tanga jana.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.

Kaimu
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Tanga,
Emmanuel Masika akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa
kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akizungumza wakati wa hafla ya
kufuturisha wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
iliyofanyika mkoani Tanga.
Mmoja wa wastaafu akitaka ufafanuzi kutika kwa viongozi wa shirika hilo kuhusu huduma za shirika hilo.
Mstaafu wa NSSF, Edith Lumeya akiuliza swali kuhusu malipo ya wastaafu.
Meneja
wa Mafao wa NSSF, James Oigo akijibu maswali ya baadhi ya wastaafu
waliotaka ufafanuzi kuhusu huduma mbalimbali za shirika hilo.
Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Wastaafu.
Baadhi
ya wastaafu wa NSSF Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya
Tanga, Halima Dendego (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufuturisha
wastaafu hao iliyoandaliwa na NSSF.

Baadhi ya wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati).
Baadhi ya wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati).
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati), wa pili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa (wa tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Maryam Muhaji.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu, (kushoto) akishiriki futari.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (wa pili kushoto) akiwaongoza akinamama kupata futari.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (wa tatu kushoto), akishiriki katika futari iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga pamoja na wadau wake. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu na wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Chiku Matesa.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (kulia), akishiriki katika futari iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga pamoja na wadau wake. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu na Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Chiku Matesa.
Wastaafu na wadau wa NSSF Mkoani Tanga wakijumuika katika futari.
Waastaafu wa wadau wa NSSF Mkoani Tanga wakijumuika katika futari.
Wastaafu na wadau wa NSSF Mkoani Tanga wakijumuika katika futari.
Baaadhi ya wadau wa mfuko huo wakipata futari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akiwashukuru Wastaafu na Wadau waliohudhulia futari iliyoandaliwaa na mfuko huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akiwashukuru Wastaafu na Wadau waliohudhulia futari iliyoandaliwaa na mfuko huo.
Watoto wanaoishi katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Barabara ya 7 Mkoani Tanga wakiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika futari iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya Wastaafu na Wadau wa Mfuko huo iliofanyika mkoani Tanga.
Watoto wanaoishi katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Barabara ya 7 Mkoani Tanga wakiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika futari iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya Wastaafu na Wadau wa Mfuko huo iliofanyika mkoani Tanga.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu akiomba dua.
Principle
Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akigawa zawadi kwa wastaafu wa
NSSF wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika hilo.
Ofisa
Mwandamizi wa Operesheni wa NSSF, Lydia Ignace akitoa zawadi kwa
wastaafu wa Shirika hilo waliohudhuria hafla ya kufuturisha
iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
Principle
Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akitoa zawadi kwa mstaafu wa
NSSF, Bella Antao wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu wa Shirika
hilo.
Na Elizabeth Kilindi, Tanga
SHIRIKA la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limejipanga kuhakikisha linaboresha mfuko huo
kwa kuwafikia wakulima na wafugaji nchini kote ili kupanua wigo kwa wanachama
wake.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa, wakati akizungumza
katika hafla ya kufuturisha wastaafu (PENSHENI) pamoja na wadau wa mfuko huo iliyofanyika
katika hotel ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Alisema kuwa
wakulima na wafugaji wamekuwa wakisaulika
hivyo kama shirika limeona vema kuwafikia ikiwemo kuwapatia elimu ambayo
itawasaidia kujiunga na mfuko huo.
‘Sisi kama shirika tumeona itakuwa ni vizuri zaidi
kuwafikia wakulima na wafugaji ili kuweza kujiunga na mfuko wetu ambao unamafao
uzazi, kuumia kazini, Kustaafu na mengineyo'.
Kaimu Mkurugenzi
huyo alisema shirika limeanzisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanachama wake
kupitia Saccos ambapo utalenga kuwawezesha wanachama wa mfuko huo kujikwamua kiuchumi.
Naye Mkuu wa Wilaya Tanga Halima Dendego aliwataka wafanyakazi waliojiajiri na walioajiriwa
ikiwemo wa mashambani kujiunga na mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF ili kuweza
kujiwekea akiba hasa ya uzeeni.
“Nawaasa
hawa wafanyakazi wajiunge na mfuko huu kwani unafaida kubwa hasa unapostaafu
unakuwa na uhakika wa kuishi maisha bora yasiokuwa na wasiwasi’’alisema Dendego.






























No comments:
Post a Comment