Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Raymond,akitoa elimu kwa viongozi na wawakilishi wa Talgwu ngazi ya kata na mkoa,kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii CHF kwenye ukumbi wa kanisa katoliki la Mt. Francisi Axvery mkoani Lindi.
Mgeni
rasmi kwenye kikao kilichoambatana na mafunzo ya mfuko wa taifa wa bima
ya afya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Vijijini bi Oliver
Vavunge,ambapo aliwataka wawakilishi wafanyakazi kuwakumbusha kutimiza
wajibu ili maslai yaweze kuboreka sanjari na kusisitiza kuwa watambue
NHIF ina msaada mkubwa kwao na kwetu kama waajiriwa hivyo watumishi wa
sekta ya afya wana jukumu kubwa la kusimamia huduma ili ziboreke zaidi
kupitia fedha zinazolipwa kupitia bima ya afya,kushoto ni mwenyekiti
Talgwu mkoa wa Lindi.
katibu
wa Kamati ya uratibu Talgwu Mkoa wa Lindi ndg kambogoro Rashidi akitoa
taarifa ya madhumuni ya mkutano wa mwaka wa viongozi na kamati ya
uratibu na utoaji wa elimu kutoka NHIF kwa mgeni rasmi ambaye ni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi Vijijini Oliva Vavunge.
Washiriki wakimsikiliza kwa makini hayupo pichani meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Bi Fortunata Raymond,ambapo aliweka bayana makusudio ya ofisi ya Mkoa wa Lindi ilivyoweka mkakati wa kutoa elimu inayohusu umuhimu na faida za kujiunga na mifuko ya afya ya jamii(CHF), sanjari na maboresho ya kitita cha mafao cha NHIF kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment