Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amempa muda wa miezi miwili
mkandarasi anayejenga barabara ya Ndundu-Somanga kufanya kazi usiku
na mchana ili kumaliza kazi hiyo haraka bila kutoa visingizio vyovyote.
Waziri wa Ujenzi aliitoa kauli hiyo leo katika kijiji cha Manzese, Wilayani
Kilwa mkoani Lindi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la
ujenzi.
Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa mkandarasi huyo ameshalipwa fedha
zote alizokuwa ana dai hivyo anachotakiwa ni kufanya kazi kila siku usiku
na mchana ili amalize kazi hiyo haraka
“Tunataka mpaka mwezi wa tisa, tuone barabara ya lami na sio vinginevyo,
wahandisi wote wa mkoa wa Pwani na Lindi wamsimamie kwelikweli na
kwa muda wote ili aweze kukamilisha kazi hii kwa muda tuliompa” Alisema
Waziri Magufuli
Pia waziri wa Ujenzi aliwaasa Wananchi kutomwibia Mkandarasi huyo
Mafuta ili aweze kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
“Msiibe mafuta kwa mkandarasi pia nayeye anatakiwa awalipe vizuri
wafanyakazi wake kwasababu sisi pia tunamlipa vizuri, pia anatakiwa
atunze vifaa vyake vizuri” alisema Waziri Magufuli.
Kuhusu barabara ya kutoka Lindi kuelekea Mtwara katika baadhi ya
maeneo, Waziri Magufuli amewataka viongozi wa mkoa kusimamia malori
yanayobeba gipsam na mawe makubwa kupita kiasi hali inayohatarisha
usalama wa barabara hiyo.
“Nawataka msimamie hili pamoja na TANROADS ikiwezekana waweke
mizani inayohamishika kupima malori hayo. Hii itasaidia kulinda barabara
zetu ambazo tunatumia fedha nyingi kuzijenga” Alisema Dkt. Magufuli
Kuhusu udongo unaodondoka katika eneo la Mchinga, Waziri Magufuli
alisema katika mwaka huu wa fedha, wizara imetenga bajeti kwa kazi hiyo
ya kutengeneza eneo hilo ili tatizo lisiendele.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akipiga
ngoma jana mkoani Mtwara kabla ya Ufunguzi wa Barabara ya Masasi
–Mangaka na uwekaji wa jiwe la msingi wa barabara ya Mangaka –
Mtambaswala 71.5km.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakwanza
kulia akipita juu ya daraja la Nangoo Wilayani Masasi wakati wa ukaguzi
huku akifatiwa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale,
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mhandis Mussa Iyombe pamoja na
Mwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Africa (ADB) Bi Tonia Kandiero.
Sehemu ya barabara ya Ndundu Somanga kama
inavyooneka baada ya mkandarasi kuanza kufanya kazi kwa kasi tofauti na
hapo awali.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi wa kijiji cha Manzese kuhusu Mkandarasi anayejenga barabara
katika eneo hilo la Ndundu Somanga kuwa anatakiwa ndani ya miezi miwili
awe amekamilisha barabara ya lami bila visingizio vyovyote.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
mbele ya viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Pwani na Wizara ya Ujenzi,
ADB na wakandarasi kuhusu ujenzi wa barabara ya Ndundu Somanga
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kufanya ukaguzi wa maendeleo ya
ujenzi wa barabar hiyo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana
na wananchi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Manzese katika
barabara ya Ndundu Somanga mkoani Lindi.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akitoa
maelekezo kwa mkandarasi anayejenga barabara ya Ndundu Somanga
kuhusu kumalizia kipande cha kilometa kumi kilichobakia ndani ya muda
wa miezi miwili.Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano-GCU-
UJENZI
No comments:
Post a Comment