HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 21, 2014

SHIRIKISHO LA MCHEZO WA BAO TANZANIA LA LAANI VIKALI WANASIASA WANAO WAKASHFU WAASISI WA MUUNGANO

Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa.

Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania limelaani vikali wanasiasa wanao simama na kutoa maneno ya kejeli zidi ya waasisi wa Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani kwani huko ni kutokuwa na maadili yenye sura alisi ya Utanzania.

Hayo yamesemwa na Raisi wa shirikisho hilo Bw Monday Likwepa kwenye Mashindano ya Mchezo maalum wa Bao wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani yanayo fanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

‘’ Shirikisho kwa kupitia mchezo huu na wadau wake wote wamesikitishwa na kukerwa sana na tunalaani vikali vitendo vya baadhi ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba na Wabunge wa Jamuuri ya Muungano kwa kutumia nafasi walizo pewa sasa wamegeuza na kuwatuhumu, zalilisha na kuwakashfu waasisi wa Muungano wetu Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume’’ Alisema Bw Likwepa.

Bw Likwepa aliongeza kuwa watanzania wakumbuke kuwa waasisi wa Muungano wetu walikuwa ni wanachama wa Mchezo wa Bao hivyo chama hakitokuwa tayari kuona walio kuwa wanachama wake ambao ndio wakombozi wa nchi hii wanadhalilishwa hivyo watafanya maandamano siku ya Tar 26 Aprili 2014 kuanzia Chang’ombe TCCT hadi uwanja wa Taifa mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano kwa lengo la kulaani vikali tabia hii mbaya.

Nae Mzee Jabiri Sultan Nyumba ambae alikuwa akiudhuria michezo ya Bao ya Mwl Nyerere huko kwa Mzee Shaban Kalolo Mtaa wa Jangwani amewashauri wanasiasa kuiga mfano wa waasisi wa Muungano wetu walivyo tumia muda wao mwingi kuliunganisha Taifa na si kulisambaratisha kama wanavyo taka kufanya wanasiasa wa chache hivi sasa.

‘’wanasiasa watumie Lugha nzuri zenye maelewano na kujenga kama tunavyo zitumia kwenye mchezo wa Bao, Lungha zetu uvunja itikadi za vyama, udini na Ukabila, si za ugomvi ni za kujenga, inashangaza sana kuona wanasiasa wanakosa busara, nivyema tukatatua matatizo yetu kwa busara’’ aliongeza Mzee Nyumba.

Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure amesema kuwa wataendelea kuuwenzi mchezo wa Bao kwa kuifadhili Shirikisho hili la Bao nchini kwa kulipatia mahali pa kufanyia shughuli zao, kwani wanatambua mchango wa Mchezo huu katika Ukombozi wa Taifa letu.

Michuano hii ya Mchezo wa Bao wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania imeshirikisha Timu 13 za hapa jijini Dar es Salaam na itafungwa rasmi Tar 26 Aprili na Waziri wa Uchukuzi Mh Harrison Mwakwembe na Mshindi wa kwanza atajinyakulia Tsh 500,000/=, wapili Ths 300,0000/= na watatu Tsh 200,000/=.
Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure (katikati) akimsikiliza kwa makini mmoja wa Makamisaa wa Mchezo wa Bao na kulia ni Mzee Jabiri Sulutan Nyumba.
kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure (katikati) akifuatilia kwa umakini mchuano mkali kati ya mchezaji wa Nyayo na Mzinga.
timu mbali mbali zikiumana vikali katika michuano ya Bao ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, inayo endelea katika ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
wachezazi wa Timu mbali mbali wakifuatilia matokeo ya awali ya mchezo huo wa Bao inayo endelea katika ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad