Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani katika viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam.
Wakipita kwa shangwe mbele ya meza kuu huku wakihamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Wakiwa na furaha ya kuadhimisha siku ya wanawake ambayo kauli mbiu yake ilikuwa ni chochea mabadiliko chanya ili kuleta usawa wa kijinsia.
Meneja Matekelezo wa NHIF, Grace Lobulu akifurahia namna watumishi wa Mfuko walivyopita mbele ya meza kuu.
Baada ya kutoka kwenye maandamano, watumishi wa Mfuko walitumia fursa hiyo kwenda katika Hospitali ya Ocean Road kwa lengo la kuwaona wagonjwa na kuwapa pole.
Wanawake wa NHIF wakibeba vitu kwa ajili ya kuwashika mkono wagonjwa.
Wakielekea katika wodi za wagonjwa
Wakijadili jambo kabla ya kuingia wodini
No comments:
Post a Comment