Mhasibu mkuu wa Samsung Tanzania Bw. Ibrahim Kombo (Kulia) akikabidi zawadi kwa mshindi wa mwezi Januari wa huduma ya e-warranty Bw. Sherali Faril wakati wa hafla fupi yya makabidhiano ya zawadi mbalimbali kwa wateja waliojishindia bidhaa za Samsung kwa droo ya mwezi Januari baada ya kununua simu halisi ya Samsung.
Baadhi ya washindi wa Samsung e-warranty katika picha ya pamoja na Mhasibu Mkuu wa Samsung Tanzania Bw. Ibrahim Kombo (wa pili toka kulia) mara baada ya tukio la kukabidhi zawadi kwa washindi hao waliojinyakulia bidhaa mbalimbali toka Samsung baada ya kununua simu halisi za Samsung na Kuzisajili katika mfumo wa e-warranty ikiwa ni njia yya kupambana na bidhaa feki.
Kampuni ya Samsung Tanzania kitengo cha elektroniki hivi leo imetangaza washindi wa draw wa mfumo wake mpya wa E- warranty. Mfumo huu wa E-warranty inawapa wateja dhamana ya miezi 24 pale wanapo nunua simu mpya ya Samsung.Wateja wanajisajili kwa mfumo huu kwa njia ya SMS ili kujua kama simu ya ni halili au ya bandia.
Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Bwana Kishor Kumar akizungumuza na waandishi wa habari alisema ‘Wateja wanaonunua simu zetu na kujisajili kwenye e-warranty wanaingia moja kwa moja kwenye draw ya kujishindia zawadi mbali mbali’.
Washindi wanaweza kushinda zawadi 1 kati ya hizi 10: Televisheni 1 aina ya LED ya inchi 32, laptop 1, Kamera 3, home theatre 3 na simu 2 aina ya Galaxy Grand.
‘Mfumo huo wa e-warranty unawasaidia wateja kujua kama simu ya Samsung wanayotaka kununua inadhamana ya miezi 24, kama simu imeibiwa au inatafutwa na kama simu ni mpya au imeshatumika’, Bwana Kumar aliendelea kusema.
Kujua kama simu ni halali, mteja anatakiwa kufuta maelekezo yafuatayo: Tuma ujumbe na neno ‘Check’ ikifuatiwa na alama ya nyota (*) kisha namba ya IMEI, ikifuatiwa na alama ya reli (#) na kutuma kwa namba ‘15685’. Ujumbe unatumwa moja kwa moja kuelezea hadhi ya simu hiyo ya Samsung.
‘Mfumo huu wa e-warranty ulianzishwa haswa kukabiliana nan a changamoto moto inayoikumba soko la simu za mkononi huku Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, ambapo kuna simu nyingi ni za bandia, za wizi, zilizotumika na simu ambazo hazina dhamana’, alisema Bwana, Kumar.
Bwana Kumar alimaliza kwa kusema ‘ili kuboresha huduma zetu za mfumo wa e-warranty, wateja watakaonunua simu aina ya Galaxy S 4 (iliyozinduliwa mwezi huu jijini Dar es Salaam), watapata huduma mpya inayoitwa ADH. ADH (Accidental Damage from Handling), ni huduma inayoilinda simu hiyo ya S 4 kutoka uharibifu kutokana na matumizi ya kawaida’.
Ilikujiunga na huduma ya ADH, wateja wanatakiwa kujisajili na mfumo wa e-warranty na usajili untakiwa kufanywa ndani ya siku 30 tangu kununuliwa kwa simu. Athari ya kutokujiunga na mfumo wa e-warranty kwa muda unaotakikana ni kwamba simu hiyo ya S4 haitaweza kutengenezwa kwa bure pale ambapo itaharibika.
No comments:
Post a Comment