Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akikabidhi Kombe kwa Jaji Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma nchini,Lawrence Salva,litakalokabidhiwa kwa Mshindi wa Kwanza wa Safari Lager Nyama Choma,Wakati wa Uzinduzi wa Mashindano hayo jijini Dar es Salaam leo.anaeshuhudia katikati ni Mratibu wa Shindano la Safaro Lager Nyama Choma,Peter Zacharia.
Meneja
wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (kushoto) akisisitiza jambo
wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dar es Salaam wakati wa kutangaza Uzinduzi rasmi wa Mashindano ya Safari
Lager Nyama Choma 2014,ambapo amesema kuwa lengo kuu la Shindano hilo
ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa Nyama Choma ili kwa
pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa
Nyama Choma.Kulia ni Jaji Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma
nchini,Lawrence Salva.
Jaji
Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma nchini,Lawrence Salva (kulia)
akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kwamba katika zoezi hilo
la kumsaka mchoma nyama bora hapa nchini,kuwa kutakuwa na vigezo mbali
mbali vitakavyotumika kufanikisha zoezi hilo,ambapo alivitaja baadhi ya
vigezo hivyo kuwa ni Usafi wa Mazingira,Vifaa vya Kufanyia Kazi,Joto
Maalum ya Uchomaji Nyama na vingine vingi.
Taswirazz
Mratibu
wa Shindano la Safaro Lager Nyama Choma,Peter Zacharia (kushoto)
akisisitiza jambo wakati akitaja mikoa itakayoshiriki kwenye Shindano
hilo,ambayo ni Mbeya,Mwanza,Kilimanjaro na Jiji la Dar es Salaam.Kulia
ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (kushoto) pamoja na Jaji Mkuu wa Mashindano ya Nyama Choma nchini,Lawrence Salva wakikata moja ya nyama iliyokidhi viwango vya kuliwa na mlaji wakati wa uzinduzi rasmi wa Mashindano ya Safari Lager Nyama Choma uliofanyika leo jijini Dar.







No comments:
Post a Comment