Mshindi wa tuzo za mitindo na mbunifu aliyetamba na mavazi ya single button kwa takribani miaka miwili sasa Martin Kadinda anategemea kuanza ziara ya kuonyesha mavazi yake katika nchi kubwa za kiafrica.
Kadinda amesema kuwa kwa mwaka huu amepanga kufanya maonesho yake nje ya nchi kwa sana kwakuwa huko ndio kunaitangaza nchi na brand yake kwa ujumla.
Show yake ya kwanza kwa mwaka huu itakuwa Nchini kenya katika Jiji la Nairobi usiku wa tar moja akiwa na wabunifu kutoka tanzania na nchi nyingine za africa Katika SWahili fashion week Kenya... baada ya kenya safari itakuwa ni Lusaka Zambia ambapo huko atakwenda kuonesha mavazi yake mapya mwishoni mwa mwezi wa tano.
Akizungumzia nguo atakazozionesha kadinda anasema Supremacy ni mavazi mchanganyiko ikiwepo africa shirt ambazo anaziita kwachkwachu kama anavyoonekana pichani.. pia suti zenye vitambaa vya linean and hazitakuwa na solid colour kama ilivyokuwa kwa single button.



No comments:
Post a Comment