HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 14, 2014

MAMLKAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) NA MAMLAKA YAUSAFIRI WA ANGA NCHINI CHINA (CAAC) WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA NDEGE ZINAZOTENGENEZWA CHINA KUTUA KATIKA ANGA LA TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi na Mkurugenzi Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China (CAAC)Li Jian wapili kutoka (kulia) wakisaini mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo Ndege zinazotengenezwa nchini China  zitaruhusiwa kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa jijinia Dar es Salaam, utawawezesha Mamlaka hiyo hapa nchini kuweza kujenga kwa wataalam kuweza kudhibiti Ubora wa Ndege hizo kutoka China. Kutoka Kushoto ni Mwanashereia wa TCAA Vallery Chamulungu na Kulia ni Executive Vice President of Aviation Industry Corporation of China (AVIC) Mr. Geng Runguang.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi na Mkurugenzi Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa China (CAAC)Li Jian (kulia) wakikabidhiana hati za mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo Ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa leo katika katika Makao makuu ya ofisi hiyo jijinia Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe Kutoka nchini China waliohudhuria hafla ya utiliwaji mkataba wa ushirikiano wa maswala ya Usafiri wa Anga , ambapo Ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutua katika Anga ya Tanzania. Mkataba huo uliosainiwa jijinia Dar es Salaam, utawawezesha wataalam wa TCAA kudhibiti Ubora wa Ndege hizo kutoka China.
Viongozi wa kuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga China (CAAC) wakiwa katika Picha ya Pomoja baada ya kusaini mkataba wa Ushirikiano wa maswala ya usafiri wa anga ambapo ndege zinazotengenezwa nchini China zitaruhusiwa kutuoa katika anga la Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad