IGP Mstaafu Said Mwema akiwa katika Gari Maalum la wazi huku akipunga mikono kwa Maafisa, Askari, Wageni Waalikwa na Wananchi mbalimbali katika hafla fupi iliyofana sana ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma. Sherehe hizo zimefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
IGP
Mstaafu Said Mwema(kushoto) akimkabidhi kitara IGP Mpya wa Jeshi la
Polisi, Ernest Mangu(kulia) ikiwa ni ishara ya Makabidhiano ya Madaraka
ya Uongozi wa Jeshi la Polisi hapa Nchini. Sherehe hizo zilizopambwa na
Gwaride Maalum lililounndwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi
imefana sana katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakipunga mikono wakati IGP Mstaafu, Said Mwema(hayupo pichani) akipita katika Gari Maalum la wazi. Hafla hiyo fupi imefanyika kwa ajili ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma(wa Nne toka kulia) ni Mkrugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid(tatu toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile).
IGP
Mstaafu, Said Mwema akipokea Salaam ya heshima na utii iliyotolewa na
Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la
Polisi(hawapo pichani) katika hafla fupi ya kumuaga rasmi kufuatia
kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria. Hafla
hiyo imefanyika leo Februari 15, 2014 katika Viwanja vya Polisi barracks
Jijini Dar es Salaam.
IGP
Mstaafu, Said Mwema akikagua Gwaride Maalum alililoandaliwa na Maafisa
na Askari wa Jeshi la Polisi katika hafla ya kumuaga rasmi kufuatia
kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa kumjibu wa Sheria.
Gadi
ya Wanaume iliyoundwa na Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama
Barabarani wakipita kikakamavu mbele ya IGP Mstaafu, Said Mwema(hayupo
pichani) kwa mwendo wa haraka katika hafla fupi ya kumuaga rasmi
kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa
Sheria.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi ambao walijitokeza kwa wingi
katika hafla fupi iliyofana sana ya kumuaga rasmi IGP Mstaafu kufuatia
kustaafu kwake Utumishi wa Jeshi la Polisi kwa mujibu wa Sheria. Sherehe
hizo zimefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barrack Jijini Dar es
Salaam.
Wanakikundi rafiki wa Ulinzi Shirikishi wakipiga makofi wakati IGP Mstaafu Said Mwema(hayupo pichani) akipita katika Gari Maalum la wazi wakati wa hafla fupi ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma. IGP Mstaafu Said Mwema atakumbukwa hapa Nchini kwa namna alivyoshirikiana na Wananchi pamoja na Wadau wa Amani katika dhanaya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii.
IGP Mstaafu Said Mwema(wa pili kushoto) akipongezwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja baada ya hafla fupi iliyoandaliwa na Uongozi wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kumuaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma kwa mujibu wa Sheria. Hafla hiyo fupi iliyofana sana imefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks Jijini Dar es Salaam.
IGP Mstaafu Said Mwema akiagana na Kamishna wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve mara baada ya hafla fupi ya kumuaga rasmi. Hafla hiyo imefanyikia katika Viwanja vya Polisi Barracks leo Februari 15, 2014 Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje).










No comments:
Post a Comment