| Ijumaa ya February 22 majira ya 7 kasoro dakika kadhaa nawasili kijiji cha Mijongweni wilayani Hai. |
| Safari yangu hii ni kutizama maenedeleo ya Bib Aziza Mohamed aliyekuwa akiishi chooni baada ya nyumba yake kuezuliwa na mvua yenye upepo mkali ghafla milangoni nakutana na kufuri. |
| Hata pale nilipomwacha siku ya kwanza kufika ,Chooni ambako bibi huyo alihamishia makazi yake pia kulikuwa na kufuri. |
| Nikalazimika kwenda kwa mtendaji wa Kitongoji cha Kijiweni Abdul Msuya kupata msaada wa kumpata Bi Aziza na safari ya kumtafuta ikaanza. |
| Njiani tunakutana na maeneo ambayo yaliathirika na maji ,yakiwemo mashamba ya migomba ,mahindi kadharika mpunga. |
| Mwenyekiti Msuya alinionesha kila mahala palipo pata athari ya mvua hiyo. |
| Migomba iliharibika vibaya. |
| Udongo ulizolewa na kupelekwa kwenye mashamba ya Mpunga. |
| Hata ndizo
zilizokuwa tayari zimebeba pia ziliharibika vibaya . |
| Hata Bamia ikalazimu kina mama kukata mashina ya bamia na kugeuza kuni. |
| Tarajio la kuuvuna mahindi pia limeingia dosari. |
| Baada ya safari ya takribani nusu saa kwa mbaali namuona Bi Aziza Msuya . |
| Alikuwa akiotesha maharage shambani kwake. |
| Baada ya kusalimiana ikamlazimu kumalizia kwanza kuzika mbegu kwa mashimo aliyokuwa amechimba tayari. |
| Tukaianza safari ya kurejeas nyumbani kwake kwa kuifuata reli. |
| Safari ilikuwa ni ndefu kiasi . |
| Mwendo ukaongezeka mwenyekiti wa kitongoji Bw Msuya mbele ,Bi Aziza nyuma. |
| Dakika 45 zinakamilisha safari yetu na hatimaye tunafika nyumbani kwa Bi Aziza. |
| Bi Aziza anachukua funguo na kufungua moja ya chumba katika nyumba iliyoezuliwa na upepo. |
| Ghafla anatoka ndani na furushi ,baada ya kumuuliza hicho nini,kwa unyonge anasema ni matandiko ya mtoto wake Sikujua Aloyce mwenye mtindio wa ubongo. |
| Anafungua chumba kingine . |
| Baadae anatoka na fungua ameshikilia mkononi anaelekea kilipo choo. |
| Anafungua kufuri la mlamngo wa Chooni. |
| Kuanzia hapo nalazimika kuvuta tofali na kuligeuza kama kigoda kisha nikaanza mahojiano na Bi Aziza. |
| Tulizungumza mengi pembeni akiwepo mwenyekiti wa kitongoji cha Kijiweni Msuya akisikiliza kwa makini maelezo ya Bibi zaidi akieleza kuwa alikuwa akiishi katika choo hicho hadi siku hiyo. |
| Bi Aziza alinieleza kuwa sehemu hiyo ni sehemu ambayo hulala mtoto wake Sikujua ,lakini nyakati za mchana hugeuka jiko. |
| Chumba hiki kipo katika nyumba iliyoezuliwa isipokuwa sehemu ya paa lilibaki na kuweka japo kivuli cha mbali. |
| Chumba/Jiko. |
| Bado nikawa na maswali tena hapa chooni kwa Bi Aziza zaidi kuhusu Afya yake hakuona kama ni tatazo. |
| Bi Aziza ananieleza ni tatizo kubwa huku akikiri kuwa ndani ya choo hicho kuna mbu wa kutosha na sasa ameanza kusumbuliwa na MARALIA |
| Natoa pole kwa Bi Aziza kisha naweka mikono yangu nyuma kisha narudi sehemu yangu ya kazi. |

No comments:
Post a Comment