Mkurugenz Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akionyesha kwa waandishi habari kipeperushi cha huduma ya Hatoki mtu hapa wakati wa uzinduzi,ambapo wateja watapa vifurushi vya BURE Packs vya kutuma pesa bure kwa wiki au Mwezi. Halfa ya huduma hii ilifanyika katika Makao makuu ya Airtel Leo.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza rasmi huduma ya kisasa ya
kifedha kupitia huduma ya Airtel Money. Huduma hiyo mpya ya kibunifu
itatoa uzoefu tofauti wa huduma za fedha kwa wateja wake.
Akiongea
wakati wa uzinduzi , Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwana Sunil Colaso
alisema "leo tunayofuraha kuzindua huduma yetu mpya ya Airtel Money
ijulikanayo kama "Hatoki Mtu Hapa", kwa mara ya kwanza nchini Tanzania
wateja wa Airtel watafurahia kufanya miamala bure bila kikoma kwa
kununua kifurushi cha Bure Pack cha wiki au cha mwenzi."
Vifurushi
vya Bure Packs vitawapa wateja wa Airtel Money uhuru wa kuchagua
kifurushi kinachokidhi mahitaji yao na kuwawezesha kufanya miamala bure
bila kikomo kwa wiki au kwa mwenzi kulingana na matakwa yao.
Tumezindua
huduma hii ili kuwapatia wateja wetu ubora, urahisi na unafuu katika
kufanya miamala ya pesa.Kwa wateja ambao hawatajiunga na virufushi vya
Bure Pack bado wataweza kufanya miamala ya pesa kwa bei nafuu kuliko
zote ambapo kwa sasa watatozwa asilimia 50% yaani nusu bei ukilinganisha
na gharama zinazotozwa na mitandao mingine.
Tunauhakika
wateja wetu watafaidika sio tu kwa ubora, urahisi na ufanisi wa huduma
yetu ya Airtel Money bali kwa kupata huduma zenye viwango nafuu zaidi,
Akiongea kuhusu jinsi ya kupata huduma hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
Airtel Bi Beatirce Singano Mallya alisema "kujiunga na "Hatoki Mtu
Hapa" packs wateja watalipia 1500 mara moja tu na kuendelea kufanya
miamala bure bila kimomo kwa wiki nzima, vilevile watakaojiunga kwa
mwenzi watalipia shilingi 5000 na kuendelea kufaidi huduma bure kwa
mwenzi mzima".
"kwa
ubunifu huu mpya huduma ya Airtel money bado itawawezesha wateja kupata
huduma nyingine za ziada. Sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kununua
vifurushi vya Airtel Yatosha kwa namba zao au kwa namba ya mtu mwingine
mahali popote , wakati wowote kupitia huduma ya Airtel money,"
aliongeza.
Huduma
ya "Hatoki Mtu Hapa" ni kwa wateja wote wa Airtel nchini , na kwa
wateja wapya watakachotakiwa kufanya ni kutembelea Ofisi za Airtel au
mawakala wa Airtel Money zaidi ya 35,000 walioko nchi nzima na kununua
simcard mpya kisha kujisajili wakiwa na kitambulisho rasmi na kufurahia
huduma.
Huduma
ya Airtel Money imesaidia kuondoa changamoto za huduma za kibenki
vijijini na mijini ambapo imewawezesha wateja kutuma na kupokea pesa
bure, kulipia Ankara mbalimbali kama ada za shule, Visa ya US, bili ya
maji DAWASCO, Umeme LUKU pamoja na DSTV. Ili kujiunga na huduma ya
Airtel Money, Mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kupata Menu ya Airtel
Money.


.jpg)
No comments:
Post a Comment