Askari polisi wakikusanya nguo za ndani katika soko la Meiomoria wakati wa operesheni ya kukamata wauzaji wa nduo hizo zilizopigwa marufuku.
Askari polisi akimsindikiza mwanamke mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja baada ya kukutwa akiuza nguo za ndani zilizopigwa marufuku katika soko la Meimoria mjini Moshi.
Mmoja wa wauzaji wa nguo za mitumba katika soko la Meimoria akiwa amejificha chini ya meza ya kuuzia nguo kukwepa askari polisi pamoja na maofisa wa shirika la viwango Tanzania (TBS) wakati wakifanya operesheni ya kukamata wauzaji wa nguo za ndani.Mwananmke huyo alitoka chini ya meza baada ya kubembelezwa na wenzake hata hivyo wakati askari polisi akimtaka kwenda kupanda gari la polisi mwanamke huyo alikimbilia tena chini ya meza hiyo,askari polisi wakalazimika kumucha.
Mama huyo akijieleza mbele ya Polisi.
Mmoja wa wauzaji wa nguo za ndani akiingia kwenye gari la polisi baada ya kukutwa akiuza nguo za ndani.
Askari polisi akimuhoji mmoja wa wauzaji wa nguo za ndani,juu ya uwepo wa nguo hizo katika stoo yake ya kuhifadhia Marobota ya nguo za mitumba.
Operesheni ikiendelea Stoo moja baada ya nyingine ambapo jumla ya Marobota matano yalikamatwa na kisha kuteketezwa katika dampo la Kaloloeni.
Mmoja wa wauaji wa nguo za ndani,akiwa mikonoi mwa polisi muda mfupi baada ya jaribio la kuwakimbia askari kushindikana.
Marobota yaliyokamatwa katika soko la Meimoria yakipakiwa katika gari tayari kwenda kuchomwa katika dampo la Kaloleni. Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jami,Moshi.
SERIKALI MUHIMU HAPO KWAHIZO NGUO ZA NDANI ONDOENI USHURU KWA HIZO NGUO ZA NDANI MPYA ILI ZIPUNGUEBEI MADUKANI ILI KILA MWANANCHI AWE NA UWEZO WA KUNUA DUKANI NA PIA KWA ANAE TAKA NGUO HIZO KUZITOA TENA NNJE YA NCHI ATOZWE USHURU KWA KUTOA NNJE YA NCHI,HILO MUHIMU SANA ZAIDI YA HAPO MTAKUWA MNAWANYIMA HAKI WANANCHI, MAANA HIVI SASA ZA MADUKANI HAWAWEZI KUZINUNUA KUTOKANA NA BEI NA UWEZO WAO
ReplyDelete