HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 22, 2014

TAARIFA YA KIFO CHA MBUNGE WA CHALINZE

Marehemu Mhe. Saidi Ramadhani Bwanamdogo
(Mbunge wa Chalinze)

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Saidi Ramadhani Bwanamdogo (Mb), kilichotokea Asubuhi ya leo (Jumatano) tarehe 22 Januari, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili/ MOI alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Mipango ya Mazishi inaendelea kufanywa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho siku ya Alhamsi tarehe 23 Junuari, 2014 kijijini kwake MIONO, Wilaya ya BAGAMOYO, Mkoa wa PWANI. Taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kadri zitakapopatikana.
“Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un”
Imetolewa na

Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
22 Januari, 2014

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad