HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 1, 2014

salamu za mwaka mpya 2014

Salaam aleikum kwenu Wadau wetu wapendwa.

Timu nzima ya Michuzi Media Group Ltd (MMG)ambao ni wamiliki wamitandao pendwa ya kijamii ikiongozwa na Libeneke la Globu ya Jamii Michuzi Blog,Jiachie Blog na Mtaa kwa Mtaa Blog pamoja na ile ya Michuzi Matukio, inawatakia Heri ya Mwaka Mpya wa 2014 Wadau wote popote pale mlipo,kwa kuwa pamoja na timu hii kwa kipindi chote tangu timu hii ilipoanza kuingia mitamboni miaka kadhaa iliyopita.

Kwakweli tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na Ardhi kwa kuweza kutufanikisha kuuona Mwaka huu Mpya wa 2014 tukiwa hai na wazima wa afya,kwani kuna wenzetu wengine hawajaaliwa kufika siku hii,hivyo kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu,tunapaswa kumshukuru sana.

Timu nzima ya Michuzi Media Group Ltd (MMG)inawatakieni kila la kheri katika Mwaka huu mpya wa 2014 na Mwenyezi Mungu atujaalie sote uwe ni mwaka wa mahanikio kwa kila mmoja wetu.

Ahsanteni sana

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad