Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kukagua maonyesho ya vijana wajasiriamali ya mkoa wa morogoro akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni iliyoandaa maonyeshi hayo Ndugu Jackson Audiface. Maonyesho hayo ambayo yapo katika mpango wa kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana ujulikanao kama Tanzania Youth Entrepreneurship Programme (TAYEP) ambao upo chini ya kampuni ya AJ IT Development Company Ltd.
Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akikagua baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka mkoa wa morogoro. baadhi ya vijana hao kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine, Chuo kikuu Mzumbe, Chuo kikuu cha kiislaam Morogoro. Lengo la maonyesho hayo ni kuzitangaza na kuzitafutia masoko kazi za vijana wajasiriamali.

No comments:
Post a Comment