HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 25, 2014

Mh. Mhagama afungua Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) jijini Dar

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Jenista Mhagama (kushoto) akigawa zana za kazi kwa mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Primus Mkwela baada ya kulifungua baraza hilo jijini Dar es Salaam jana Ijumaa Januari 24, 2014. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa TET, Dk Leonard Akwilapo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Jenista Mhagama (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Profesa Idris Kikula ( katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk Leonard Akwilapo, wakati naibu waziri huyo alipofungua Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) jijini Dar es Salaam jana Ijumaa Januari 24, 2014.
Vicheko na nderemo vilitawala wakati Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Jenista Mhagama (katikati) alipokwenda kufungua Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na kukutana na wenzake waliosoma naye na kufanyakazi ya kufundisha miaka mingi iliyopita. Naibu Waziri huyo alikuwa mgeni kwenye uzinduzi wa baraza hilo la TET jijini Dar es Salaam jana Ijumaa Januari 24, 2014.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad