Kwa Jina naitwa Osman Bairu ni Mwanamichezo na Mwalimu wa Mchezowa Kriketi (Cricket),Nilianza kucheza mchezo huu wa Kriketi nikiwa na umri wa miaka sita(6) nilipokuwa nchini India katika shule ya msingi iitwayo Barnes school.
Nilipokuwa shuleni India nilivutiwa na timu ya Taifa ya WEST INDIES na mchezaji aitwae VIVIAN RICHARDS ambaeni Keptein wa timu ya taifa ya WEST INDIES.
Katika kipindi cha Mwaka 1984 Nilifanikiwa kucheza katika timu ya shule katika nchi ya Panchigan -1996 Nilikuwa na timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka kumi na saba(17) mjini Mombasa,nchini Kenya na baadae mwaka 1998 Nilikuwa na timu ya taifa ya Tanzania-Uganda nikiwa Mwafrika peke yangu.
Mwaka 1996 nilipata kushinda na kuwa mchezaji bora wa kuchipukia kutoka katika chama cha Kriketi (Cricket) Tanzania nikiwa Mwafrika wa kwanza. -Nina cheti cha ushiriki katika Kriketi kutoka Alayans Kriketi ligi ya Tanzania.
-Tumeshinda kikombe cha Mwl.Nyerere kapu nikiwa na timu ya jimkana Kriket klab.
Nimeamua kuuendeleza mchezo wa Kriketi (Cricket) kwa vijana wa umri mdogo ambalo ndilo jambo ninalofanya kwa wakati huu e.g
(i) Nina klabu yangu mwenyewe chini ya umri wa miaka kumi na tano(15) iitwayo Dar Raptors sport klabu
(ii) Ninajitolea kuwafundisha vijana wa shule ya Msingi Kawe ambao wasichana walishashinda kikombe cha chanzo kriketi kapu (Cricket Cup) mwaka 2010 katika ya shule za msingi kumi na nne(14). Katika mashindano hayo msichana aitwae Diana Jane mwenye umri wa miaka kumi na mbili(12) alipata kikombe cha mchezaji bora.
(iii)Dar Raptors klabu 208 nilipata kombe la mshindi wa pili katika ligi ya Kriketi (Cricket) chini ya umri wa miaka kumi na sita(16) na 2009 tukawa mabingwa kwenye ligi ya umri mdogo.
Kwa kweli mchezo huu wa Kriketi unachangamoto nyingi sana kwa hapa nchini,baadhi ya changamoto hizo ni Vifaa vya mchezo wa Kriketi (Cricket) ni vigumu kupatikana kwake hapa nchini hadi kuagiza nje,Viwanja kwa ajili ya mchezo wa Kriketi (Cricket) ni haba sana,Inakuwa ni vigumu kwa washiriki wenye asili ya Kiafrika kwa Dhana ya kuwa washiriki walio wengi ni wafrika wenye asili ya Kiasia
Ombi langu kubwa kwa Serikani ni kusaidia kupatikana kwa uwanja wa Mchezo huu wa Kriketi (Cricket) wenye hadhi ya kimataifa pamoja na urahisi wa upatikanaji wa vifaa vya mchezo wa Kriketi (Cricket).
Mchezo huu wa Kriketi (Cricket) upate kipaumbele kama mchezo wa mpira wa miguu uwe unafundishwa mashule Tanzania nzima, mafunzo yatolewe kwa walimu wa mchezo huu na zawadi zitolewe katika mashindano kama kivutio kwa washiriki.
Wadau wajitolee na wahamasishe kwa hali na mali.
Mchezo huu wa Kriketi (Cricket) uanzie chini pawepo na mashindano ya mara kwa mara ligi za ndani na nje kwa shule za msingi,kwani utaweza kuinua vipaji vya watoto wengi hapa nchini.
Mdau Osman Bairu (wa nne kulia waliosimama) alipokuwa na timu ya Taifa ya Mchezo wa Cricket nchini Uganda.
Mdau Osman Bairu akiwa na moja ya timu zake za mchezo wa Kriketi (Cricket) mara baada ya kutaa ubingwa wa mchezo huo kwa timu za shule ya msingi.
Akiwa na timu ya Kawe B.








No comments:
Post a Comment