kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imefanya ziara ya Tathmini ya siku tatu katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Tanga na kuridhishwa na utekelezaji wa Mfuko wa maendeleo ya wanawake kwani umesaidia wanawake wengi kujiendeleza na kupambana na umasikini unaomkabili mwanamke, kamati hii ilipita katika vikundi vya wanawake wajasiriamali na kushuhudia shughuli wanazo zifanya kutokana na mkopo walioupata kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF).
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe Sofia Simba (kulia) akieleza mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii mafanikio yaliyopatikana.
Mjasiliamali akijieleza mbele ya kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii mafanikio aliyoyapata kutokana na mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF).

.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment