HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 13, 2013

Watu 6 wapoteza maisha baada ya kuangukiwa na kifusi huko mkoani kilimanjaro

 Wananchi wakijaribu kuangalia cha kufanya ili kuweza kufukua udongo na kuopoa miili ya watu walofukiwa na kifusi katika machimbo ya Moramu eneo la Pumuani wilaya ya Moshi vijijini huku wananchi wengine wakishuhudia.
Uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro ukiongozwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama ukishuhudia zoezi la ukoaji wa miili ya watu hao.
Mmoja ya mwili wa mmoja kati ya watu sita waliokufa kwa kufunikwa na kifusi katika machimbo ya Moramu eneo la Pumuani wilaya ya Moshi vijijini.
Gari aina ya fuso lenye namba za usajili T 167 AQG ambalo marehemu wa tukio hilo walikuwa wakijaza Moramu likiwa limeangukiwa na ngema iliyokatika na kusababisha vifo vya watu sita.
Wauguzi wakiendelea kutoa msaada kwa watu waliofunikwa na kifusi hicho.
kamati ya ulinzi na usalama ilikuwepo hadi usiku wa saa nne jana hadi shughuli ilipo malizika.
Greda ya manispaa ikijaribu kubeba gari lililoangukiwa na gema ili zoezi la uokoaji miili uendelee kwa urahisi.
 uokoaji ukiendelea.
Miili ya marehemu waliofukiwa na kifusi ikitolewa katika udongo baada ya kazi ya zaidi ya saa 5 ya kufukua eneo hilo kumalizika.
Baadhi ya ndugu wa marehemu walizimia baada ya kuona miili ya ndugu zao ikiopolewa kutoka kwenye udongo. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad