HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 16, 2013

WAFANYAKAZI DAWASCO WAHIMIZWA KUONGEZA UFANISI KATIKA KAZI

Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO, Eng Jackson Midala amewataka wafanyakazi wa shirika lake kuongeza ufanisi wa kazi ili kufikia malengo ya shirika katika kutoa huduma bora na inayokidhi viwango.

Nasaha hizo amezitoa wakati akitoa zawadi mbalimbali za ngao na pesa taslimu kwa wafanyakazi na vituo vilivyofanya vizuri katika makusanyo ya shirika kwa mwezi October na November ambapo aliwahimiza kuongeza juhudi zaidi ili malengo yaliyopangwa na shirika yaweze kufikiwa.

Eng Midala alibainisha kuwa jumla ya Tsh Bil 44/= zipo mikononi mwa wateja kama MADENI na hivyo ni wajibu wa wafanyakazi kuyafatilia ili yaweze kulipwa kwa wakati. Alisema kuundwa kwa kamati ya Makusanyo ya Shirika kutasaidia kufuatilia madeni kutoka kwa wateja wakubwa na wadogo wa DAWASCO ambao wanalimbikiza madeni kwa muda mrefu licha ya kupata huduma ya Maji.

Sherehe za DAWASCO za kuwatunuku wafanyakazi waliofanya vizuri hufanyika kila jumamosi ya mwanzo wa Mwezi ili kutambua mchango wao kwa maendeleo la Shirika.

Wakati huo huo Eng Midala ameweka Mkataba wa Makubaliano wa Kazi kwa Meneja wote wa Dawasco walio katika kanda / vituo 13 ndani na nje ya Jiji la Dar. Mkataba huo ni sehemu ya makubaliano ya kuongeza ufanisi na kuhakikisha DAWASCO inajikwamua ili kuweza kupunguza nakisi iliyopo. Aliwaomba wafanyakazi wote kutoa ushirikiano kwa Meneja wa vituo ili waweze kutekeleza mpango huo.
Afisa mtendaji Mkuu wa Dawasco,Eng Jackson Midala (Mwenye miwani) akisema machache kabla ya kuanza kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali waliofanya vizuri katika makusanyo ya Shirika kwa mwezi Octoba na Novemba .kutoka kulia ni Meneja Ufundi wa Dawasco Eng Shabani Mkwanye na Afisa Biashara Mkuu wa Dawasco Ndugu Jamal Ally.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng.Jackson Midala akikabidhi cheti kwa mshindi wa jumla wa makusanyo(Revenue) ya Shirika kwa mwezi October kwa Meneja wa Dawasco BagamoyoTumain Mhondwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Eng Jackson Midala akitoa kombe la ushindi kwa Meneja wa Dawasco Kinondoni, Ainea Kimaro baada ya kituo chake kuibuka mshindi wa thamani ya Makusanyo (Collection Value) kwa Mwezi wa November.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Eng Jackson Midala  akitoa zawadi ya trophy na pesa taslimu Tsh 100,000/=kwa mshindi wa mwezi October aliyefikisha malengo ya makusanyo (Target Perfomance) kutoka kituo cha Kibaha.
Picha ya pamoja kati ya Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco Eng Jackson Midala (wa tatu kushoto) na mameneja wa vituo vya Dawasco 13 vilivyo kwenye kanda mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es salaam baada ya utiaji saini wa Mkataba wa Kazi. Sherehe hii fupi ilifanyika katika ofisi za Dawasco Makao Makuu. (Picha zote na mdau Everlasting Lyaro wa Dawasco)

1 comment:

  1. wezi wakubwa dawasco, inakuwaje wanampa mteja bili ambayo hajaitumia? kwamfano:- leo ni tar.10./12 wanakuja kusoma mita halafu wanakuprintia papo hapo bili ya kuanzia tar. 10/12 - 30/12 je hayo maji nimeyatumia saa ngapi na sijafikia hiyo tar? je kama ntasafiri kesho yake na familia yangu nyumba tukaifunga je ntatumia hayo maji saa ngapi? si wizi huu? kwa nini wanakisia bili? mimi nyumbani kwangu kwa mwezi 1 sifikii sh. 14,000 lakini sasa hiv napewa bili ya 40 - 45 kwa mwezi!! kwakweli nawashangaa sana dawasco! hatukubali llazima tuwalipue clouds! huu ni wizi wa wazi kabisaaaaa.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad