Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na maswala ya kuhamasisha watu mbali mbali kujisomea (Community Reading Association),ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo,Bi. Zahra Rashid (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi hiyo ulifanyika jana kwenye Bustani ya Hoteli ya Kebby's,Bamaga jijini Dar es Salaam.Wengine walioshiriki kushika utepe huo kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo,James Dongwe,Mweka Hazina,Farida Sekimonyo pamoja na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,Bi. Jerida Swedi.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na maswala ya kuhamasisha watu mbali mbali kujisomea (Community Reading Association),ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo,Bi. Zahra Rashid akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi la Taasisi hiyo.
Furaha baada ya Uzinduzi.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,Bi. Jerida Swedi akizungumza machache mbele ya wageni mbali mbali waliokuwepo kwenye Uzinduzi huo juu ya Mwenendo wa Taasisi yao hiyo mpya.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,Bi. Jerida Swedi akigawa vitabu kwa wadau mbali mbali waliofika kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakijisomea.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment