Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli (kulia) akizungmza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kuzungumzia namna ya kuendesha kampeni ya kuwalinda wanyama Tembo,ambao wanazidi kutoweka kutokana na kuuliwa kila siku na majangili.Mkutano huo umefanyika leo kwenye Ukumbi wa Safari Pub,Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Mahusiano wa TBL,Edith Mushi.
Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Mil 10,kwa mwakilishi wa mfuko wa Pams Foundation, Maximillan Jenes ambao ndio wanaoongoza kampeni hiyo ya kupiga vita mauaji wa Tembo nchini.Katikati ni Meneja Mahusiano wa TBL,Edith Mushi.
BIA ya Ndovu imetoa kiasi cha Sh milioni 10 kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kuwalinda tembo, wanyama ambao wanazidi kutoweka kutokana na kuuliwa kila siku kwa ujangili.
Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli alisema, fedha hizo zimepatikana kutokana na kampeni kubwa iliyokuwa ikiendeshwa kwa kushirikisha Watanzania, katika kueneza habari za umuhimu wa uhifadhi wa tembo.
“Bia ya Ndovu ilianza ushirikiano na asasi ya Pams Foundation kwa lengo la kuelimisha na kuisaidia jamii katika juhudi za kulinda wanyama, hasa tembo ambao karibu kila siku wanauawa 30 kwa njia ya ujangili.
“Zoezi hili la kukusanya fedha na kuwaelimisha Watanzania kwa ujumla tumelifanikisha na leo hii tunakabidhi kiwango hiki cha fedha taslimu kwa Pams Foundation. Ni tumaini letu kuwa fedha hizi zitatumika kama zilivyokusudiwa kwa ajili ya faida ya kutoa elimu na kununua vifaa vya kusaidia kuwalinda wanyama hao,” alisema Pamela.
Akipokea msaada huo, mwakilishi wa mfuko huo, Maximillan Jenes alisema, fedha hizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kuhakikisha ujumbe na elimu juu ya kulinda wanyama hao unawafikia wengi, ikiwa pia kununua vifaa mbalimbali vya kwa askari wanyamapori wanaopambana kuwalinda.
“Watanzania pia tunapaswa kubadilika na kuweka mikakati ya kuwalinda tembo waliobaki hapa nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho, pia tunawashukuru Ndovu kwa msaada wao huu,” alisema.
Naye Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi alisema, hiyo ni sehemu ya kampeni za kampuni hiyo kuhakikisha inashirikiana na jamii katika kuwalinda tembo.
“Bia ya Ndovu imefanikisha na itaendelea kufanikisha kusambaza ujumbe kwa jamii juu ya uhifadhi wa tembo na kuwapa Watanzania imani kubwa ya kuweza kukabiliana na changamoto hii.”
Bia ya Ndovu inazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:
Post a Comment