Ili kupanua Wigo na uelewa wa Hifadhi ya Jamii ,hivi Karibuni Mamlaka ya Usimamaizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii iliendesha Elimu kwa umma kuhusu Kazi na Majukumu ya Mamlaka ( SSRA), umuhimu wa sekta wa hifadhi ya Jamii na wananchi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, Sekta ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, changamoto na muelekeo wake.
Akifungua semina za mafunzo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Ludovick John Mwananzila aliipongeza Mamlaka kwa kuchukua hatua ya kuutembelea mkoa wa Lindi na kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii, kwani wananchi wengi hawana uelewa juu ya Hifadhi ya Jamii, kiasi cha wengi wao kufananisha kustaafu na kifo. Aliishauri Mamlaka kuiagiza Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kuhakikisha inatoa Elimu ya kutosha kwa wananchi wote na hasa mikoani, kwa wananchi wengi hawana Elimu hiyo.
‘’Wananchi wote wakijiunga na mifuko ya hifadhi ya Jamii watakuwa na maisha na si bora tu badala yake maisha bora na marefu zaidi maana watakuwa hawana wasiwasi wote” alisema .
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii imeundwa kwa sheria Na. 8 ya 2008 ,kama ilivyorekebishwa na Sheria Na.5 ya mwaka 2012, Jukumu kuu likiwa ni Kusimamia na Kuboresha utendaji wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini pia kulinda, kutetea na kuendeleza maslahi ya wanachama wa sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Mkuu wa mkoa wa Lindi wa kwanza Kushoto, Ras wa Mkoa wa Lindi wa pili kushoto, Mkurugenzi wa sheria SSRA kushoto na mkuu wa mawasiliano na uhamasishaji SSRA kabla ya kuanza semina ya mafunzo kwa viongozi wa mkoa wa Lindi.
Viongozi wa Mkoa wa Lindi na Taasisi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Ludovick Mwananzila akifungua semina ya Mafunzo.
Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi Bi. Tusekile Mwaisabila akiuliza swali na kutoa maoni mara baada ya mada za mamlaka kuwasilishwa .
Picha ya Pamoja na Mkuu wa MKoa Katikati, RAS wa kwanza kushoto, DC kushoto ,wafanyakazi wa SSRA na baadhi ya Wajumbe waliohudhuria semina ya mafunzo.
Wajasiria mali wa Mkoa wa Lindi Wakimsikiliza Mkurugenzi wa sheria wa SSRA Bw. Ngabo Inbrahimi akiwasilisha mada ( Hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment