HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 6, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AKIFUNGUA MKUTANO WA HIGH LEVEL GROUP KUHUSU ELIMU NA AFYA KWA VIJANA WA NCHI ZA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini ya Afrika wa UNAIDS na Mwenyekiti wa High Level Group Profesa Sheila Tlou wakati wa ufunguzi wa mkutano wa High Level Group unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 6.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa siku mbili wa High Level Group, unaofanyika huko Cape Town tarehe 6 na 7, Desemba 2013. Mkutano huo unazungumzia masuala ya elimu na afya kwa vijana wanaoishi katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wa High Level Group wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kanda wa UNAIDS, Profesa Sheila Tlou na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa siku mbili wa High Level Group, unaofanyika huko Cape Town tarehe 6 na 7, Desemba 2013. Mkutano huo unazungumzia masuala ya elimu na afya kwa vijana wanaoishi katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.
 Baadhi ya wajumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa High Level Group wakimsikiliza Mama Salma Kikwete aliyekuwa akifungua rasmi mkutano huo. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mheshimiwa Radhia Msuya tarehe 6.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza kijana Remmy Shawa, mjumbe wa High Level Group mara baada ya kutoa mada yake 'Background to the East and Southern Africa Commitment Process' kwenye mkutano wao wa siku mbili unaofanyika Cape Town nchini Afrika Kusini tarehe 6.12.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad