HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 6, 2013

MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL AOMBOLEZA KIFO CHA MZEE MANDELA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Afrika ya Kusini Masaki jijini Dar es salaam leo Disemba 6-2013, kufuatia kifo cha Rais wa Zamani wa Afrika ya kusini Mzee Nelson Mandela (95) aliyefariki Dunia jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi na Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania Henry Thanduyise Chiliza kwenye ofisi ya Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini Dar es salaam leo Disemba 6-2013, wakati alipofika kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha Rais wa Zamani wa Afrika ya kusini Mzee Nelson Mandela (95) kilichotokea jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania Henry Thanduyise Chiliza kwenye ofisi ya Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini Dar es salaam leo Disemba 6-2013, wakati alipofika kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha Rais wa Zamani wa Afrika ya kusini Mzee Nelson Mandela (95) kilichotokea jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad