HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 21, 2013

Bondia Alibaba wa Kilimanjaro atamba kumpiga Kaseba kwa KO

Bondia Alibaba Ramadhani wa mkoani Kilimanjaro (shoto) akizungumza na Mdau Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea jijini Dar es salaam jana kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Bondia Japhet Kaseba litakalo fanyika kesho.

Na Dixon Busagaga,Moshi.

BONDIA Alibaba Ramadhani wa mkoani Kilimanjaro ametamba kumpiga kwa Knock out (KO) bondia Japheth Kaseba wa jijini Dar es Salaam.

Alibaba alitoa kauli hiyo jana muda mfupi kabla ya kupanda gari kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya shughuli ya kupima afya na uzito itakayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Friends Corner leo saa 4 kuelekea mpambano wao wa kesho.

Akizungumza kwa kujiamini Alibaba amesema amaefanya maandalizi ya kutosha na yuko tayari kuwashangazza mashabiki wa mchezo huo watako jitokeza katika kushuhudia mpambano huo hiyo kesho.

Pambano hilo linalofanyika kwa uratibu Ibrahim Kamwe wa Kampuni ya Bigright Promotions ya Dar es Salaam kwa kivuli cha PST, litasindikizwa na mengine sita likiwemo la Karage Suba na Fadhili Awadh ‘Tiger’ katika uzani wa welter kg 66 watakaozichapa kwa raundi kumi.

Akizungumzia pambano hilo la kesho, Kamwe amesema wengine watakaopima uzito leo ni Mbarouk Heri atakayezichapa dhidi ya Lusekelo Daudi na Issa Omar Nampepeche ataoneshana kazi na Hassan Kiwale ‘Moro Best.’

Naye Zumba Kukwe atazichapa na Jacob Maganga; Adam Yahya vs Harman Shekivuli, Jocky Hamis v Mbena Rajab, Ernest Bujiku na Shah Kasim, Shaban Kitongoji v Mwinyi Mzengela, Shaban Manjoly v Kassim Chuma.

Aidha, bondia mwingine wa Tanzania anayeishi nchini Canada, Kareem Kutch, atacheza na Tata Boy kwa pambano la kimataifa la Kickboxing la raund tano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad