Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo mbalimbali wanaotarajiwa kufanya mahafali yao kesho tarehe 29, Novemba 2013 katika chuo hicho. Waziri Nchimbi alitoa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Gerald Monela. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza (CGP) John Minja na Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Profesa Peter Gillah.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpa cheti
mwanafunzi Nuru Ally aliyefanya vizuri kuliko wanafunzi wote katika somo
la Development Studies katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
kilichopo mjini Morogoro. Mwanafunzi huyo pia alikabidhiwa zawadi ya
Shilingi 50,000. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma SUA, Profesa
Peter Gillah.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wapili kushoto aliyevaa tai) wakiwa katika picha ya pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri karika msomo mbalimbali wanaotarajiwa kufanya mahafali yao kesho tarehe 29, Novemba 2013 katika chuo hicho. Waziri Nchimbi alitoa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika msomo mbalimbali chuoni hapo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:
Post a Comment