Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr. Syrivia Mamkwe akizungumza katika mkutano wa uanzisshwaji wa mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA) katika Manispaa hiyo. Mpango huo unasimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Betha Minga akifungua mkutano huo.
Ofisa Sheria wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Matilda Kagombora akitoa salaam za wizara kwa wadau wa TIKA.
Wadau wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo.
Sehemu ya wadau wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi iliyosisitiza umuhimu wa kujiunga na Mfuko huo.
Diwani wa Kata ya Temeke Bw. Sombo Shaaban akisalimia wadau wa mkutano huo.
Sehemu ya wadau wa mkutano huo
Ofisa Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Grace Michael akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr. Syrivia Mamkwe wakati mkutano ukiendelea.
WANANCHI wa Manispaa ya Temeke wametakiwa kuchangamikia mpango wa Tiba kwa Kadi mara tu utakapoanza kwa kuwa unalenga kupunguza gharama za maisha hususan za matibabu ambazo zimekuwa zikiongezeka kila kukicha.
Rai hiyo imetolewa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Bi. Betha Minga katika uzinduzi wa mkutano wa wadau ambao watajadili na kupitia michakato mbalimbali ya uanzishwaji wa mpango huo ndani ya Manispaa ya Temeke ili kuruhusu kuanza kwa mpango huo.
“Mpango huu ni mzuri sana hakuna asiyefahamu gharama za matibabu zilivyo kubwa na zinavyopanda kila kukicha na kwa hapa Temeke niseme tu kwamba tumechelewa sana hivyo suala hili tulipeni uzito wa aina yake ili tuanze mara moja,” alisema.
Aidha aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanajadili mpango huo kwa umakini mkubwa na kwa kuzingatia maslahi chanya ya wananchi wa Manispaa ya Temeke na kuepukana na malumbano ambayo yatachangia kuchelewesha uanzishwaji wa mpango huo.
Naye Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA) Bw. Constantine Makala aliwaeleza wajumbe hao kuwa, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mpaka sasa imeshaendesha mpango huo katika Manispaa mbalimbali zikiwemo za Morogoro, Pwani, Ilala, Kinondoni, Njombe na maeneo mengine.
Alisema kuwa mpango huo ni wa nafuu kwa wananchi kwa kuwa uchangiaji wake ni wa mara moja kwa mwaka hivyo akahimiza viongozi wote kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha wanahamasisha wananchi kuchangamkia mpango huo.

No comments:
Post a Comment