Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu taarifa ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa inayohudumia wakimbizi ( UNHCR). Katika mchago wake, Balozi Mwinyi pamoja na Mambo mengine alieelezea uzoefu wa Tanzania katika kuwapokea, kuwahifadhi na pia mchakato wa kuwarejesha makwao kwa hiari wakimbizi baada ya hali ya usalama kutengemea. Pia alisifu ushirikiano mzuri ulipo katika ya Tanzania na Shirika hilo. Taarifa ya UNHCR inaelezea kwamba kwa kipindi cha mwaka jana watu 1.1 milioni walizikimbia nchi zao kutoka na sababu mbalimbali ikiwamo vita na machafuko kiasi cha kuliongezea mzigo Shirika hilo wakimbizi hao wanatoka katika nchi za DRC, Mali, Sudan/Sudan ya Kusini na Syria.
Kwa taarifa zaidi soma hapo chini

No comments:
Post a Comment