MINI ZIFF 2013 inafanyika sambamba na Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar. Tamasha hili dogo litafanyika tarehe 10 -12 Jan, 2014 na kama kawaida
ZIFF itatoa tuzo 10 za Filamu kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2013 katika filamu
za Kiswahili (Bongo Movie).
Tuzo zitakazotolewa ni Muigizaji Bora wa Kiume na
Kike, Muongozaji Bora, Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji anayechipukia, Filamu
bora katika Sauti, Filamu bora katika Hadithi, Balozi bora wa Filamu za kitanzania,
Kampuni au mtu aliyetoa mchango mkubwa katika Tasnia hii kwa mwaka huu na
Tuzo ya Heshima. Tamasha hili dogo litajumuisha filamu za kitanzania peke yake
(Bongo movies) ilikuendelea kutoa mwamko kwa watengenezaji filamu wa Tanzania
kufanya vyema katika tasnia hii, Tamasha hili ni utangulizi wa tamasha kubwa la ZIFF
litakalofanyika 14 – 22 Juni, 2014.
Tuzo zitatolewa baada ya jopo la majaji kupitia kazi zilizoletwa kwaajili ya Mini ZIFF
na pia Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Kike zitapata kupigiwa kura na wananchi
kupitia namba maalum itakayotolewa hapo baadae kupitia Puch Mobile na hivyo
kufanya watu wote Tanzania nzima kupiga kura.
Mini ZIFF itaonesha filamu kwa siku mbili na siku ya mwisho Tuzo zitatolewa kwa
walioshinda, pia tunategemea kuwaalika wasanii mbalimbali maarufu kutoka hapa
Tanzania kama JB, Cloud, Steve Nyerere, Ray, Makombora, Simon Mwakifamba,
Monalisa, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Lulu na wengine wengi.
Pia tunategemea kufanya show kabambe ya muziki baada ya kutolewa kwa tuzo,
wasanii watakaopanda jukwaani watatangazwa hapo baadae. Kwa wale wote
wanaotaka kuleta kazi zao basi walete sasa ila ziwe ambazo zimetoka mwaka 2013
tu. Wasiliana na Ibra 0713300997(DAR) au Mohd 0778685676 (ZNZ).
MINI ZIFF 2013 inaletwa kwa udhamini mkubwa wa ZUKU, Push Mobile, Azam
Marine, Filamu Central Clouds TV kupitia kipindi cha Take One na Clouds FM kupitia
kipindi cha Leo Tena.


Zitafanyika wapi Iringa au Songea au Dodoma
ReplyDelete