Mkurugenzi wa Kampuni Frontline,Hellen Kiwia (kulia) akizungumza na Waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika mapema leo,wakati akitoa tathmini ya Safari ya Baadhi ya Waandishi wa Habari pamoja na Mbunifu wa Mavazi,Sheria Ngowi ya kwenda Nchini Afrika Kusini kwa mualiko maalum kutoka Bodi ya Utalii ya nchi hiyo,ambapo walihudhulia Maonyesho ya Mavazi ya Mercedes Fashion Week 2013 yaliyofanyika Jijini Pretoria pamoja Utalii wa Maeneo mbali mbali nchini humo.Wengine pichani ni baadhi ya Wandishi waliokuwepo kwenye safari hiyo pamoja wadau.
Mie nikiwa ni mmoja wa wanahabari tuliofanya ziara nchini afrika kusini nikizungumza machache kuhusiana na safari hiyo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Duka la Mavazi la Sheria Ngowi,lililopo Mtaa wa Bizwagi,Masaki jijini Dar es Salaam.Kiukweli tulijifunza mambo mengi sana kutoka kwa wenzetu wale,ikiw ni pamoja na namna wenzetu wanavyotoa kipaupembele kwenye swala zima la Utalii.
Picha ya Pamoja ya Wadau walikwenda nchini Afrika Kusini hivi karibuni.





No comments:
Post a Comment