Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kimepania kuunga mkono jitihada za Serikali ya kuhakikisha elimu inaboreka hapa nchini, DUCE kwa mara nyingine imepokea wanafunzi ambao watasomea Diploma ya juu ya Elimu, diploma hii inawalenga wale ambao hawana taaluma ya ualimu.
Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam Dkt. Kitila Mkumbo akitoa maelekezo kwa wanafunzi wapya wa Diploma ya Juu ya Elimu ambao wanaanza masomo mwezi huu, kozi hiyo ni maalum kwa watu mbalimbali wanaofundisha lakini hawana taaluma ya elimu. Kushoto ni Naibu Mkuu wa chuo anayesimamia masuala ya Taaluma Profesa Godliving Mtui na kulia ni Kaimu Mshauri wa mwanafunzi Bibi. Upendo Mlugusye.
Baadhi ya wanafunzi wapya wakijitambulisha wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Diploma ya Juu ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment