Wizara ya Maji ikishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya mbalimbali zimepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa kwa kuwapatia maji safi wanakijiji 752,000 kwa kipindi cha miezi mitatu.
Baadhi ya miradi iliyo kamilika ni pamoja na ile inayohusisha Vijiji vya Mtandi, Rondo, na Kineng’ene vilivyopo Mkoani Lindi; Vijiji vya Engagile, Gedamar, Mtuka vilivyopo Mkoani Manyara; na Vijiji vya Iwalanje, na Maninga vilivyopo Mkoani Mbeya.
Katika utekelezaji wa mfumo wa MMS, Wizara imegatua na kugawanya madaraka kwa Secretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya, jambo ambalo limewafanya watendaji kuwajibika na kuharakisha utendaji wao wa kazi za kila siku. Katika utekelezaji wa MMS, Wizara ya Maji imefanikiwa kuongeza ufanisi katika masuala ya ununuzi wa huduma, ikiwemo ujenzi na vifaa vyake, kutoka siku 265 za hapo awali hadi siku 90 za sasa.
Aidha Afisa Mwandamizi katika Wizara hiyo, Mhandisi Goyagoya Mbenna, alisema “Mpango huu wa MMS umetuwezesha sisi Wahandisi kufanya kazi kwa umakini na umeleta mafanikio katika kuharakisha utendaji wetu wa kazi”.
Hapo awali idadi ya wananchi walikuwa wakipatiwa huduma ya maji safi vijijini ilikuwa ni kati ya 300,000 -500,000 kwa mwaka. Kwa kupitia mfumo huu wa MMS, tangu tarehe 1 Julai hadi kufikia mwezi Septemba 2013, wanakijiji 752,000 wamepatiwa maji safi, baada ya kutelekeza ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 3,008 na kundwa vyombo vya watumia maji 200.
Kwa upande wake Bwana Omari Issa, Mtendaji Mkuu wa PDB alisema, “Nimefurahi sana kuona utaratibu huu wa MMS umepokelewa vizuri na watendaji na wananchi. Nawashauri wahusika wote waendelee kuutekeleza mfumo wa MMS.”
Hadi kufikia mwezi Septemba 2013, jumla wakazi 15,952,000 vijijini wanapata huduma hiyo ya maji safi. Wizara ya Maji itatekeleza jumla ya miradi 1,810 (sawa na vituo 26,720 vya kuchotea maji) na kuunda vyombo vya watumia maji 2,728 nchi nzima kwa kipindi cha miaka mitatu. Miradi hii itazidisha usambazaji wa maji kwa wakazi 7,100,000 waishio vijijini.
Akizungumzia mafanikio hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Bashir Mrindoko amesema “Utelekazaji wa mradi katika mfumo wa MMS itawezesha idadi ya wakazi waishio vijijini wanopata huduma ya maji safi ifike 23,000,000 ifikapo Juni 2016. ”
Mara kwa mara Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amekuwa akiwataka wafanyakazi wa sekta ya maji kuhakikisha wanaongeza jitihada katika kazi sambamba na kwenda na kasi ya MMS. Wizara ya Maji kwa upande wake inashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Secretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya kusimamia na kufuatilia utekelezaji ili kujiridhisha kuwa miradi ya Maji inatalekelezwa kwa kiwango kilichowekwa.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Dk. Binilith Mahenge akipima msukumo wa maji katika uzinduzi wa kituo kipya cha kuchotea maji Wilayani Monduli Arusha.
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe akiwa katikati ya wanakijiji wakichota maji katika uzinduzi wa kituo kipya cha kuchotea maji Mtwara vijijini.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Dk. Binilith Mahenge na Bwana Steven A Steven, Meneja -Mamalaka ya Maji Safi and Usafi wa Mazingira – Mwanga wakikagua kisima kirefu kilichokamilika ujenzi wake hivi karibuni wilayani Mwanga Kilimanjaro.
Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe akipewa maelezo juu ya mitambo ya kusukumia maji na Bwana Mansour Mandemla, Meneja- Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Makonde katika ziara aliyoifanya wilayani Newala Mtwara.
Waziri ya Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Bwana David Nuntufye, Meneja - Mamalaka ya Maji Safi and Usafi wa Mazingira- Masasi Nachingwea wakikagua mabwawa ya maji mradi wa maji wa Masasi Nachingwea Wilayani Masasi Mtwara.

.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
No comments:
Post a Comment