Juzi katika pita pita zangu nilisimama kidogo pale Quality Plaza ili nichukue pesa kidogo Bank kwa ajili ya sikukuu, cha kushangaza nilichokikuta baada ya kutoka tu Bank ndani ya dk 10 nikakutana na lundo la vijana wa NPS wakidai ushuru wa Parking!!! Nikajiuliza hivi hawa vijana wametokea wapi?? Mbona sijawahi kuwaona kipindi cha nyuma?? Na nikajiuliza tena hizi parking si za mwenye jengo?! Ila sikupata majibu ya maswali yangu wakati huo huo nilisikia watu wakisema mpaka wafanyakazi wa maeneo ya hilo jengo pia wanadaiwa ushuru wa parking ambao ni Tsh 300/= kila siku kwa saa.
Basi nikaondoka zangu nikiwa njiani nikakutana nao tena maeneo ya Jamana wametapakaa wengi saana ikionesha waziwazi ni ulaji wa mtu fulani na kawaweka pale kwa makusudi kabisa ya kutengeneza pesa!! Basi nikaelekea Uchumi Supermarket maana nilikuwa nimetoa pesa mwanzo ili niende kufanya shopping hapo...Kufika Uchumi Supermarket Quality Centre baada ya muda na kutoka nje wakati wa kuondoka tena nakutana nao wakidai tena pesa!! tena kwenye parking ambazo zimejengwa na mwenye jengo kwa mara nyingine tena!!!
Swali langu wadau hivi hawa watu wapo kwenye maeneo haya kisheria?? Je ni sahihi kutoza ushuru wa Parking kwenye maeneo ambayo yamejengwa na mwenye jengo?? Je haya maofisi na makampuni makubwa yaliyopo hapo kama CRDB Bank, DTB Bank, Stanbic Bank, Jamana Printers, Uchumi Supermarket, nk yanatueleza nini sisi wateja wao??? Je hizi ndio huduma bora wanazotupatia?? Maana tunawafuata wao kuwaletea business alafu tunachajiwa pesa kwa ajili ya parking ambazo wao wamepanga kwenye jengo hilo hilo!! Je sehemu kama Mlimani City Shopping Mall mbona wao hawacharge ushuru wa Parking??!!
Wahusika tunaomba mlifanyie kazi ili jambo na kutupatia majibu haraka iwezekanavyo maana huu ni wizi wa wazi wazi kwa wananchi fikiria ni Shilingi ngapi wanaingiza toka asubuhi mpaka jioni kila siku ya Mungu??!! na hatuoni faida ya hizo kodi!!! Yaani jengo ajenge mtu mwingine kodi wakusanye wao!!! Kweli haya ni majanga!!!!
WAHUSIKA TUNAOMBA MAJIBU.





No comments:
Post a Comment