Mikutano ya mwaka ya Bodi ya Magavana
ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2013
imeanza rasmi leo mjini Washington D.C. Mikutano hii itafikia kilele chake hapo
tarehe 11 – 13, mwezi Octoba ,2013.
Bodi ya Magavana wa kundi la Benki ya Dunia ( Benki ) na Bodi ya Magavana wa
Shirika la Fedha la Kimataifa ( Mfuko)
kwa kawaida hukutana mara moja kwa mwaka kujadili kazi za Taasisi
zinazowahusu. Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili
mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe. Dkt. Willium Mgimwa , Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvanus Lekwilile
pamoja na Gavana wa Benki Kuu
Prof. Benno Ndulu wao ni Magavana
wa mikutano hiyo. Nchi karibu zote zimeshawasili katika mikutano hii.
‘Lengo
la mikutano hii kwa nchi ya Tanzania, inatupa nafasi ya kuweza kujadiliana na
Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi
kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni
kutusaidia na kusikia tuna mawazo gani na maeneo gani wanaweza wakatusaidia katika
kuboresha na kuangalia kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri’. Haya
yamesemwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa alipokuwa akijadiliana na
ujumbe kutoka Tanzania.
Aidha
Mhe. Dkt. Mgimwa alisema kuwa, Katika mazungumzo na Benki ya Dunia pamoja na
Shirika la Fedha la Kimataifa, ujumbe wa Tanzania utawasilisha hali halisi ya
utendaji wa kiuchumi wa Tanzania na hali ya matumizi na mapato ya fedha na
mambo yanayohusiana na taasisi zinazoendesha nishati kama vile Shirika la umeme
Tanazania (Tanesco) na shirika la maendeleo ya mafuta Tanzania (TPDC) pamoja na
kutazama mienendo ya madeni yetu na mwenendo wa mapato kwa ujumla.
Hali ya hewa mjini hapa ni ya manyunyu na mvua za hapa na pale.
Kutoka
kushoto ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania
Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula pamoja na Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
Waziri
wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akiwa katika majadiliano na ujumbe wa
Tanzania kuhusu maandalizi ya mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la
Fedha la Kimataifa.
Kutoka
kushoto ni Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania
Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt. Silvacius Likwelile, Mkurugenzi wa Idara ya kupunguza Umasikini
MKUKUTA Bi. Anna Mwasha pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya wakisikiliza kwa makini.
Ujumbe
wa Tanzania wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na Waziri wa
Fedha hayupo pichani ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho.
Kutoka
kushoto ni Kamishna wa Idara ya Sera Bw. Beda Shallanda akiteta jambo
na Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe.
Balozi
wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akimsikiliza kwa
makini Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na
Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul
Mwafongo.Picha zote na Bi. Eva Valerian – Washington DC.
Ujumbe
wa Tanzania katika majadiliano, kutoka kushoto ni Mhasibu Mkuu wa
Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda, Kamishna Idara ya Sera Bw. Beda Shallanda,
Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe na
Bw. Said Magonya Kamishna wa Fedha za Nje akielezea jambo.
Waziri
wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Yusuph Mzee kulia, akisoma kwa makini taarifa
zitakazowasiliswa katika mikutano hiyo wengine ni wajumbe kutoka
Tanzania.

No comments:
Post a Comment