MAREHEMU BEATRICE NESTORY KAZINJA
KUZALIWA 1972 – KIFO 27/8/2013
Siku, miezi leo tarehe 27/10/2013 imetimia miezi miwili (2) tangu Mwenyezi Mungu akuite nyumbani.
Ilikuwa siku ya majonzi makuu katika familia yetu kifo kilitokea ghafla mno, ulidondoka tu wakati unajiandaa kwenda kazini na ukakata roho.
Unakumbukwa sana na familia ya Kazinja, watoto wako Ashura, Faurati, Abdul, na Mapacha Tausi na Twasin, ndugu jamaa, majirani, marafiki, wafanyakazi wenzako na wengine wote, wanakukumbuka kila mmoja kwa namna ya pekee.
Mwenyezi Mungu aendelee kuilaza roho yako mahala pema peponi, kwa watakatifu wake.
Amen.


No comments:
Post a Comment