HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 10, 2013

HP KUPIGA VITA BIDHAA FEKI KWA KUTUMIA TEKNOLOGIA YA KISASA

Meneja Masoko dhidi ya bidhaa bandia wa Ulaya,Mashariki na Kati na Afrika Bi.Tina Rose akielezea utofauti wa bidhaa za hp zilizo bandia na bora katika warsha wa bidhaa za HP jijini Dar es salaam.

Kufuatia kuibuka kwa wimbi la wafanyabishara kuuza bidhaa feki (batili), HP imekuja na teknolojia ya kisasa itakayowawezesha wateja kugundua, ndani ya muda mfupi, endapo wino za printa aina ya ‘torner’ walizouziwa ni halisi au la.


Uthibitisho huu wa programu ya HP utawawezesha wateja kugundua kirahisi machapisho ya ‘cartridge’ za ‘LaserJet’ kwa kupakua na kuweka programu ya bure kupitiawww.hp.com/go/TornerCheck, na endapo patajitokeza hali yoyote isiyo ya kawaida, watatumiwa ujumbe wa onyo na kushauriwa hatua za kuchukua.

Hivyo basi, ‘inkJet’ na ‘LaserJet’ halisi za HP na machapisho ya vipengele vya ‘cartridges za kisasa ikiwa ni pamoja na mpango mpya wa udhibiti wake mpya wa (Quick Response- QR) ambao wateja wataweza kuutumia kirahisi kupitia mtandao-wezeshi wa Smartphone au kupitia mtandao wa www.hp.com/go/ok.

Meneja Masoko dhidi ya bidhaa bandia wa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika (EMEA) wa kundi la Wachapishaji na Mifumo binafsi (PPS), Tina Rose anasema hatua ya kupambana na bidhaa bandia inaleta changamoto kubwa kwa bidhaa na ustawi wa biashara hapa Tanzania na katika mataifa mengine duniani.

“Uwepo wa bidhaa bandia unahatarisha ustawi wa wazalishaji na walaji kwa kudhoofisha viwango vya bidhaa. Bidhaa feki ni jambo baya kwa kila mmoja wetu licha ya kuzalisha mabilioni haramu ya dola na kuhatarisha sifa ya bidhaa bora kama hizi zetu. Pia inawadhuru wateja kwa kuwapatia bidhaa hafifu na kemikali zisizojulikana zinazohatarisha wachapishaji na kuharibu mazingira,” alieleza.

Aliyaongea haya katika jukwaa la siku moja lililoandaliwa na HP ili kujadili madhara ya bidhaa feki kwenye biashara na katika uchumi wa nchi kwa jumla. Tukio hili pia lilitoa fursa kwa PH kuwahabarisha wateja wake juu ya hatua wanazochukua kupambana na bidhaa bandia.

HP pia imo katika mpango wa elimu kwa umma; kuonesha na kuelimisha wateja kuhusu mpango wake mpya wa utambuzi kupitia mtandao ili kuwalinda wateja dhidi ya bidhaa haramu na za bandia.

“Vita dhidi ya bidhaa bandia inaenda ikibadilika, hatuna budi kuwa imara kupambana na ndiyo sababu kila wakati tunaboresha mbinu zetu kudhibiti bidhaa hizo katika masoko yetu duniani kote,” alisema.

Bidhaa halisi za HP zinajipambanua zenyewe kwa kuaminika na kuwa na ubora wa hali ya juu aidha, kupatikana kwa bei nafuu. Bidhaa halisi za HP LaserJet na inkjet cartridges- kinyume na bidhaa bandia- zina faida katika historia ya uzalishaji na imethibitishwa kutoa huduma bora licha ya kuleta matokeo endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad