Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohamed Bahari(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya Serikali katika kukabiliana na upungufu wa samaki nchini kwa kutoa msukumo kwa wananchi kuanzisha miradi ya ufugaji wa samaki katika maeneo yao,wakati walipotembelea mradi wa ufugaji samaki wa maji baridi katika kituo cha Edeni Fish Fam, Kilichopo Pugu Kajiungeni manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.(wapili Kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi Bahari Kuu Zahor El Kharousy(wakwanza kulia)Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Bi, Fatma Sobo.
Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Dr. Baraka Kuguru akifafanua kwa waandishi wa habari namna bora ya kukuza vifaranga vya samaki wakati walipotembelea mradi huo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakitazama moja ya mabwawa yanayotumika kufugia samaki katika mradi unaoendeshwa na William Bwemelo katika eneo la Pugu Kinyamwezi kwa msaada wa Wataalamu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

No comments:
Post a Comment