Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Wachungaji Mapambano Jacob na Charles Lugembe wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Shinyanga,Dkt. John Kanon Nkola.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini,wakati alipokuwa akiwasili kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kuendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi wa ya Kanisa hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe na kufungua pazia katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya Ufunguzi rasmi wa Jengo la Madarasa ya Shule ya awali ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo baadae aliendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi wa ya Kanisa hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipanda Mti katika eneo la Kanisa hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendesha Harambee ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo zaid ya Shilingi Milion 212 zilipatikana zikiwemo na ahadi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Dayosisi ya Shinyanga,Dkt. John Kanon Nkola akizungumza machache kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,Mh. Hamis Mgeja wakati wa harambee ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo zaid ya Shilingi Milion 212 zilipatikana zikiwemo na ahadi.
Kwaya ya Kanisa hilo kutoka Kijiji cha Segese,Ikiongoza moja ya Nyimbo za Kumtukuza Mungu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,Mh. Hamis Mgeja (kulia) akizungumza wakati wa Kuchangia harambee hiyo.
Mh. Lowassa na Marafiki zake ambao ni Wafanyabiashara Mbali mbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Michango Mbali Mbali kutoka kwa Marafiki zake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea zawadi ya kitabu cha Mungu (Biblia) kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Dayosisi ya Shinyanga,Dkt. John Kanon Nkola mara baada ya kuendesha Harambee ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo zaidi ya Shilingi Milion 212 zilipatikana zikiwemo na ahadi.
Sehemu ya Waumini kwa Kanisa hilo.



















No comments:
Post a Comment