Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa idara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. Dk Nchimbi aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam. Dk Nchimbi alifanya ziara ya siku moja katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kuzungumza na watumishi hao masuala mbalimbali ya utendaji kazi.

No comments:
Post a Comment