Bagamoyo intercollege night (BIN), tukio taaluma na burudani linaloendelea kujipatia umaarufu kwa kasi, ambalo hufanyika kila mwaka katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo linatarajia kufanyika tarehe 19 Oktoba 2013.
Kwa mujibu habari zilizopatikana leo mjini Bagamaoyo kutoka kwa msemaji wa Bodi ya Wakurugenzi wa tukio hilo Bw. Kim Kimenya, BIN kwa mara ya kwanza itashirikisha vyuo vya Bagamoyo na Dar es salaam.
Aidha zaidi ya kushirikisha vyuo vya Dar es saalam BIN itakuwa na shughuli za kijamii za kujitolea na kutembelea watu wenye mahitaji maalumu na, utoaji wa tuzo kwa wanavyuo bora kitaaluma ikiwa ni tofauti na miaka miwili iliyopita ambapo tuzo zilitolewa kwa waliopendeza yaani Lady of the night na Man of the night,walioweza kujibu maswali ya bahati pamoja na, waliong’ara kwenye michezo ya ufukweni.
Pia Kimenya amefafanua kwa upande wa shughuli za kijamii kutakuwa na usafi wa mazingira na kwa upande wa michezo kuta kuwa na mechi kamambe ya maveterani wa mji wa Bagamoyo watakaocheza dhidi ya timu ya mchanganyiko wawanavyuo.
Michezo mingine kama kuvuta kamba,riadha itakuwepo kama ilivyokuwa mwaka jana,na kwa upande wa taaluma wanafunzi bora kitaaluma kutoka kwenye vyuo shiriki ndiyo watashika dhamana za vyuo katika uwasilishaji wa mada.
Kwa upande wa burudani kama ilivyo kwa miaka iliyopita itaongozwa na msanii maarufu akisindikizwa na wasanii wengine binafsi na wasanii wa makundi ambapo msanii maarufu na wasanii wengine watajulikana mwanzoni mwa mwezi Oktoba.
Kuhusu udhamini hoteli ya Mikocheni Resort Centre (MRC) ya jijini Dar es salaan ndiyo ambayo imethibitisha kudhamini na mazungumzo yanaendelea na makampuni menginei ili yaweze kudhamini.“Ninayaomba makampuni mengine yajitokeze kudhamini BIN 2013.” alisisitiza Kimenya.
BIN inayofanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo,inaandaliwa kwa pamoja na kampuni za Kimkev entertainment,Mrimi classic wear ,na Free voice investment ltd
Sunday Mangu“ Linex” akiwapagawisha mashabiki wasomi(hawapo pichani) kwenye usiku wa BIN uliyofanyika kwenye ukumbi wa TaSuBa Bagamoyo Oktoba 12,2012.
Waliopendeza BIN 2012:
Edna Richard kutoka TaSuBa Lady of the night akiwa kwenye Pozi la pamoja na Man of the night Regan Wilnelvin kutoka chuo cha Slads mara baada ya kutangazwa kwenye ukumbi wa TaSuBa Bagamoyo Oktoba 12, 2012.


.png)
No comments:
Post a Comment