Wakazi wa Tandika Sokoni jijini Dar es Salaam, wakiwa wamefurika wakati walipokuwa wakipewa elimu ya utumiaji wa vyakula vyenye vitutubishi katika Kampeni inayoendeshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania.(TFDA) katika Wilaya za Kinondoni ,Temeke na Ilala.Mbiu ya promosheni hiyo ni kuhakikisha wananchi wanatumia vyakula vywenye nembo ya Virutubishi.
Akina mama wanaojihusisha na upembuaji wa maharage katika soko la vyakula la Tandika jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza kwa makini Adamu Juma ( kulia) wakati alipokuwa akiwapa elimu ya utumiaji wa vyakula vilivyoongezwa Virutubishi .Kampeni hiyo inaongozwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania.(TFDA) katika Wilaya za Kinondoni ,Ilala na Temeke ambapo mlaji anatakiwa kuhakikisha ananunua vyakula vilivyowekwa nembo ya Virutubishi.

No comments:
Post a Comment