Wafanyakazi
wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) leo wamefanya mgomo
wa saa chache kushinikiza Menejimenti iwalipe mshahara wao wa miezi
mitatu.
Wakizungumza
wakati wa mkutano wao wa kujadili matatizo yao ikiwemo na hatma ya
malipo ya mshahara wao wafanyakazi hao wamesema hawawezi tena kuendelea
na kazi kwani kwa sasa wana njaa ya miezi mitatu na hivyo kuitaka
Menejimenti kuwalipa kwanza mishahara yao na ndipo waendele na kazi.
Kwa upande wake Menejimenti imewataka wafanyakazi hao kuvumilia kwani tatizo lao linashughulikiwa.
Hata hivyo wafanyakazi hao wameazimia kwenda kwa Waziri Mkuu kuwasilisha suala lao.
Mmoja wa wafanyakazi wa TAZARA, Charles Sumai akiongea kwa hasira wakati wa mkutano wao huo.
Sehemu
ya abiria wanaosafiri kwa treni ya TAZARA wakiwa nje ya kituo na mizigo
yao baada ya safari ya reni iliyokuwa iwe saa 9.50 kuahirishwa mpaka
saa 2 usiku kufuatia sakata hilo leo.
Sehemu
ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wakiwa
kwenye mkutano wao kujadili matatizo mbalimbali ikiwemo hatma yao ya
kutolipwa mshahara wa miezi mitatu kuanzi Mei, juni na Julai. Mkutamo
huo ulifanyika kwenye ofisi za TAZARA, Dar es Salaam leo mchana.




No comments:
Post a Comment