SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewapongeza Wajumbe
wa Bodi ya shirika hilo
waliomaliza muda wake, kwa utendaji bora uliotukuka licha ya changamoto kubwa
walizokabiliana nazo katika kipindi chao madarakani.
Pongezi hizo zilitolewa jana usiku na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,
Dk Ramadhani Dau, wakati wa chakula cha usiku cha kuiaga bodi hiyo chini ya
Uenyekiti wa Aboubakar Rajab na kuikaribisha bodi mpya, ambayo Mwenyekiti huyo
ataendelea na wadhifa wake.
Dk. Dau alisema kuwa, ingawa kuagana ni furaha, lakini tukio
hilo pia ni huzuni kwa uongozi na wafanyakazi wa NSSF, kutokana na aina ya
utendaji na ushirikiano wa bodi hiyo na Menejimenti ya shirika hilo tangu mwaka
2010 ilipoingia madarakani.
“Menejimenti ya NSSF, inatambua na kujivunia ushirikiano
uliokuwapo baina yake na bodi hii tunayoiaga leo. Ilifanya kazi kwa weledi na
hadi inamaliza muda wake hatukuwahi kufikishana bungeni, wizarani wala
kutupiana lawama,” alisema Dk. Dau.
Aliongeza kuwa, NSSF inajivunia mafanikio na hatua
mbalimbali za mchango wa Bodi hiyo katika shughuli za Ustawi wa Jamii, ikiwamo
ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM), Daraja la Kigamboni na Barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze.
Aliongeza kuwa, anaamini bodi mpya itamalizia masuala hayo na mengine mbalimbali yaliyoanzishwa na bodi hiyo, ukiwamo mchakato wa uanzishwaji wa Tawi la Hospitali ya Apollo ya
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi iliyoagwa,
Hildegard Mziray, alisema kwa niaba ya bodi hiyo anapenda kuishukuru
menejimenti na wafanyakazi wa shirika hilo
kwa ushirikiano, lakini pia kujali na kuthamini mchango wao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau
akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Wajumbe wa Bodi iliyomaliza muda
wake na kuikaribisha bodi mpya katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Meneja Kiongozi, Uhusiano, Huduma kwa Wateja wa NSSF ,Eunice Chiume akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau baada ya kutoa hotuba yake.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF iliyomaliza muda wake, Hildegard Mziray akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa NSSF.
Meneja Kiongozi,uhusiano huduma kwa wateja wa NSSF, Eunice Chiume (kulia) akiwa makini wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau alipokuwa akizungumza.
Mwenyekiti wa bodi ya NSSF, Abubakar Rajab (kati) akifurahia jambo
BOFYA READ MORE HAPO CHINI KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA READ MORE HAPO CHINI KUONA PICHA ZAIDI
Ofisa Uhusiano Kiongozi wa NSSF, Juma Kintu akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwenyetiki wa Bodi, Abubakar Rajabu akiwaongoza wajumbe wa bodi ya NSSF kupata chakula cha jioni.
Meneja Kiongozi,uhusiano huduma kwa wateja wa NSSF ,Eunice Chiume akipata chakula.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akimkabidhi zawadi Mwenyetiki wa Bodi ya NSSF, Abubakar Rajabu.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF iliyomaliza muda wake, Hirdegard Mziray akipokea zawadi yake kutoka kwa Dk. Dau.
Baadhi ya wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao wakipokea zawadi zao.
Picha ya paamoja.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau
akiwa na Makamu Mwenyekiti mpya wa bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Zuhura
Muro na Meneja Kiongozi,uhusiano huduma kwa wateja wa NSSF, Eunice Chiume (kulia).

No comments:
Post a Comment