HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 17, 2013

MWALIMU MKUU AWAJIA JUU WAZAZI WASIOFATILIA MAENDELEO YA WATOTO ZAO SHULENI

MWALIMU mkuu wa shule ya msingi makumbusho,Mama Lyimo leo aliitisha kikao cha kujadili maendeleo ya wanafunzi shuleni hapo na hasa wale wasiojua kusoma na kuandika. 

Hii ni katika mikakati aliyojiwekea kwa kufanya mikutano ya wazazi na walimu wa madarasa mara kwa mara kujadili maendeleo ya mwanafunzi shuleni hapo.

Mama Lyimo alilaani vikali vitendo vya baadhi ya wanafunzi kutojua kabisa kusoma na pindi wazazi wanapoitwa kutotoa ushirikiano, kuhusiana na hilo ameahidi mwakani kutopokea mwanafunzi wa darasa la kwanza asiyepitia shule za awali(chekechea) na atawatimua wale wanafunzi wasiokuwa na maendeleo mazuri na wazazi hawataonesha ushirikiano.

Wakati huohuo katika kikao hicho baadhi ya wazazi walilalamikia walimu kutokuwa makini madarasani na kuwalazimisha watoto wabaki tuisheni, na kupelekea wale watoto wasiosoma tuisheni kukosa masomo kamilifu kwani masomo yote hufundishwa zaidi tuisheni na sio madarasani.
mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makumbusho akizungumza na wazazi katika kikao cha kujadili maendeleo ya wanafunzi shuleni hapo.
wazazi walioitikia wito wa kikao hicho

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad