Katibu Mkuu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= bingwa wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Sulemani Cato mara baada ya kumfunga Nahodha wa timu ya Taifa Charles Venance 4-2.Dar es Salam mwishoni mwa wiki.
Mchezaji
wa timu ya Klabu ya Mpo Afrika na Nahodha wa timu ya Taifa, Charles
Venance akicheza wakati wa mechi ya fainali dhidi ya klabu ya Sun City
wakati wa mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke
iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wachezaji wa Klabu ya Mpo Afrika wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mpo Afrika ilishinda 13-11 dhidi ya Klabu ya Sun City.


No comments:
Post a Comment