HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 16, 2013

Kili Music Tour 2013 ndani ya jiji la Mwanza jumamosi,Wakazi wa Mwanza kazi ni kwenu kwa mwendo wa Kikwetu Kwetu

 KAMPUNI ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager, inang'oa nanga kwa awamu ya pili ya Tamasha la Muziki ‘Kili Music Tour 2013’ ambapo wikiendi hii litarindima ndani ya mjini Mwanza.

Tamasha hilo ambali ni kubwa na la kipekee litafanyika Jumamosi ya tarehe 17 Agosti, 2013 mjini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba na litajumuisha wasaniii 11 watakaokonga vyema kabisa nyoyo za mashabiki wao lukuki waliopo jijini Mwanza na maeneo ya jirani.

Wasanii hao ni pamoja na Diamond, Snura Mushi, Professor J, Lady Jay Dee, Roma, Dabo, Bob Junior,Ben Pol, Kala Jeremiah, Fid Q na AT.

Matamasha ya Kili Music Tour 2013 yalikuwa yamepumzika kwa muda wa mwezi mmoja na sasa yanarejea tena kwa kishindo kwenye mikoa mitano iliyobaki.

“Tunashukuru kuwa watanzania wamelipokea vizuri tamasha hili kwa moyo mkunjufu kabisa na walishiriki kikamilifu kwenye mikoa ya Dodoma, Tanga na Kilimanjaro, tuliamua kupumzika kwa muda wa mwezi mmoja kwa ajili ya kupisha mfungo, na hii ilitupa muda mzuri wa kujipanga na kuboresha zaidi matamasha haya hivyo basi tunategemea Mwanza itajumuika nasi ipasavyo kufanikisha tamasha litakalofanyika mkoani hapo siku ya Jumamosi ya tarehe 17 mwezi huu.” Alisema George Kavishe ambaye ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro.

Bwana Kavishe aliendelea kufafanua kuwa “bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaendelea kutoa bonge la kiburudisho kwa watanzania kwa kuhakikisha kuwa kila mkoa unapelekewa wasanii mahiri kabisa wa muziki wa bongo fleva hivyo mashabiki wa muziki wakae mkao wa burudani ya Kikwetu Kwetu ambayo ndio kauli mbiu ya Matamasha yetu haya.

Kwa niaba ya wasanii wenzake msanii mahiri wa bongo fleva Professor Jay “Joseph Haule” amewataka wakazi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi huku akisema “tumejiandaa vizuri sana kutoa burudani kali kabisa, lazima mji wa Mwanza utikisike kwa kishindo cha bonge la kiburudisho kwa style tuipendayo ya “kikwetukwetu”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad